Chapati maji na shira ya embe
Tanzanian Crepes with mango syrup

By Miriam


TO read this in
English, click here
Mapishi haya ni ya chai ya asubuhi au kitindamlo cha jioni. Kwa sababu maembe ni matunda, kwa hiyo mimi naweza kusema huu ni mlo kamili wa asubuhi kama ukinywa na chai ya maziwa na maji ya machungwa kama kianzio.
Mimi sikutumi sukari wala mayai kwenye chapati maji, hii ni kwa sababu shira ya maembe ina sukari ya kutosha. Mimi nikitengeneza mapishi haya, huwa natumia nusu ya vipimo hivi. kwa sababu chapati zangu ni kama inchi 5 hivi. huwa natengeneza chapati tatu au nne.
Chapati maji  na shira ya embe

Shira ya embe (Mango syrup)
Kwanza pika shira ya maembe kabla huja pika chapati maji. Wakati shira inapoa, pika chapati.


Viungo
  • Vikombe 4........Maembe yaliyo katwa vipande vipande vidogo dogo sana. Embe liwe limeiva sana na tamu
  • kikombe ½.......Sukari
  • kipimo cha kijiko cha chai ½........iliki iliyosagwa
  • Weka vikombe viwili vya maembe, Sukari na iliki kwenye mashine ya kusaga (Blender). Saga lakini isiwe laini, acha vipande pande.
  • Weka mchanganyiko kwenye sufuria.
  • Washa moto wa kati halafu pika huo mchanganyiko. Koroga kila wakati ili usiweze kuungua au kuganda, maana sukari inaungua haraka. Acha ichemka dakika tano.
  • Punguza moto uwe moto mdogo sana. Ongeza vile vikombe viwili vya maembe yaliyobaki. Funika, pika dakika mbili.
  • Ipua weka kwenye bakuli safi. Acha ipoe.

Wakati ukisubiri shira ipoe, anza mapishi ya chapati.

 
Chapati maji (Tanzanian crepes)
Viungo
  • Kikombe 1 Unga wa ngano
  • Kikombe 1½ Maji
  1. Changanya maji na unga kwenye bakuli mbaka uwe mlaini.
  2. Akikisha kikaangio kimeshika moto vizuri, tumia moto wa kati, usiwe mkali. Nyunyizia mafuta kidogo.After the first turn
  3. Tandaza huo mchanganyiko kwenye kikaango. Rangi nyeupe ikipotea, angalia chini ya chapati kama in rangi ya kahawia nyepesi, geuza. Kama unatumia kikaango cha kawaida, ongeza mafuta kama kijiko kimoja cha chai chini ya chapati ili isinate. Kama unatumia kikaango cha kisasa ambacho hakigandishi chakula chini, basi huna aja ya kuongeza mafuta.
  4. Second turn shows
  5. Angalia kama chini ya chapati uliyogeuza ina viduara vya rangi ya kahawia nyepesi. kama inayo basi toa kwenye moto weka kwenye sahani ya mezani.

 

Hatua ya mwisho ya mapishi
1. Weka vijiko viwili au zaidi vya shira, kati kati ya chapati maji kwa urefu.
2. Kunja upande mmoja wa chapati kwenye shira.  
3. Halafu kunja upande ule uliobaki.
4. Halafu geuza chapati ili ile mikunjo isionekane
5. Ongeza Shira juu ya chapati kama picha iliyo juu ya ukurasa huu.  
Ni chakula kizuri ukila na:
  • Kunywa na chai asubuhi, au kama kitindamlo jioni na kahawa