Kashata

Mapishi ya Miriam (Mapishi ya Tanzania)

Kuna mapishi ya vyakula vitamu vingi Tanzania, na hii ni moja wapo. Lakini siwezi kuwaeleza mapishi haya yalianzishwa lini Tanzania. Lakini tunaweza kuhisi yaliletwa na watu wa Kiajemi kama vyakula vingine vya Tanzania. Kashata ni rahisi kupika na pia ni vizuri ukila kama kitindamlo na kahawa ya rangi bila sukari. Kashata za Tanzania

Viungo
  • 1 (kikombe) Maji
  • 1 (kikombe) Sukari nyeupe
  • ½ (kijiko cha chai) iliki ya kusagwa
  • 1 ½ (kikombe) Nazi mbichi iliyokunwa
  1. Changanya maji na sukari mbaka sukari yote iyayuke.
  2. Chemsha mbaka mchanganyiko uwe karibu na nusu ya ulivyoanza. Halafu ongeza iliki.
  3. Ongeza rangi na nazi. Changanya vizuri mbaka maji yote yasionekane.
  4. Toa jikoni, ipua nazi kwenye sahani halafu sambaza sawasawa. Unaweza kutumia chini ya sufuri kubonyeza juu ya nazi ili isambae vizuri.
  5. Halafu kata kama umbo la almazi au vyovyote unavyotaka.

Kula na :
•Kahawa ya bila sukari
•Kula kama kitafunio