VIBIBI / Tanzanian Rice Balls

By Miriam (Tanzanian Recipe)

Vibibi ni vitamu tamu vinavyopendwa sana Tanzania wakati wa Ramathani. Ingawa natayarisha vibi wakati wowote, watu wengi wanapenda kupika vibibi wakati wa Ramathani. Kuna jina lingine linalotumika Tanzania la vibibi, linajulikana kam vipopoo. Lakini mapishi haya yanaweza kuwa tofauti kutokana na mji unaoishi.

Tafathali kama uko nje, usitumie unga wa mchele unaouzwa madukani. Utaaribu mapishi. Nunua mchele wa jasmini, loweka halafu saga kutumia blender au coffee grinder.

Vibibi / Rice balls

Ingredients
  • 1 kikombe, unga wa mchele
  • ¼ kijiko-chai, iliki ya unga
  • 1 kikombe, tui zito
  • ½ kikombe, sukari
  • 2 vikombe, maji
  • Rangi ya chakula
  1. Chemsha kikombe kimoja cha maji .
  2. Ongeza unga wa mchele, songa vizuri na mwiko mpaka uwe mgumu.
  3. Gawa sehemu mbili au zaidi kutokana na rangi ngapi unatumia.
  4. Ongeza rangi halafu endelea kusonga mbaka uchanganyike vizuri.
  5. Tengeneza vimviringo vidogo vidogo kama 1/2 kijiko cha chai halafu weka pembeni
  6. Shira ya nazi
    • Changanya sukari, kikombe kimoja cha maji, na nazi. Hakikisha sukari imeyayuka kabisa, halafu chemsha.
    • Weka vimviringo vya mchele kwenye nazi inayochemka, acha vichemke kama dakika tano, ipua halafu endelea kupika mbaka vyote viive. Weka kwenye vibakuli vya kitindamlo.
    • Ukishamaliza kuchemsha vipopoo vyote. Ongeza moto halafu endelea kuchemsha maji ya nazi mbaka tui liwe zito kidogo kama shira nyepesi. Toa kwenye moto acha lipoe kidogo.
  7. Weka shira kwenye vibakuli vya vibibi. Unaweza kuweka shira nusu ya vibibi au jaza mbaka juu.
  8. Karibu

Serve with:
•Kula kama kitinda mlo au wakati wowote na mlo wowote.