Githeri (Mapishi ya Kenya)

Read in English
Mapishi ya Miriam
an image

Haya ni mapishi ya Kikikuyu kutoka Kenya. Ni kati ya mapishi dada yetu wa nyumba alikuwa akitupikia mara nyingi sana. Kawaida wanatumia mahindi mabichi na maharage basi. Kwa kisasa, githeri inachanganywa na kila kitu. Dada wetu wa nyumba laikuwa akipenda kuchanganya na sukuma wiki. Mchanganyiko huu ni mtamu sana na kitu kilichabakia tu, ni kuongeza nyama mezani basi, mlo wa jioni au mchana tayari.

Ingredients

  1. Changanya mafuta, Sukuma wiki, na vitunguu. pika kwenye moto wa kati.
  2. Kama vikianza kuiva, ongeza mahindi, maharage na chumvi.
  3. Punguza moto uwe kati ya moto mdogo na wa kati, funika sufuria, pika polepole mbaka chakula kiive.
  4. Weka mezani chakula kikiwa bado cha moto.