Irio na vitunguu vya kukaanga

By Miriam: Mapishi ya Kenya

Githeri ni mapishi ya wakikuyu wa Nairobi, Kenya. Haya mapishi yana athiri ya Waingereza. Waingereza walitawala Kenya kwa muda mrefu na waka wazoesha Wakenya na tabia ya kunywa chai, na pia chakula kinachojulikana kama Githeri kati ya Wakikuyu. Githeri ni viazi ulaya vilivyo pondwa na mboga za majani, mahindi mabichi, na nyama. Mimi nilikula githeri za aina mbalimbali nilipokuwa Kenya; nyingine zilipikwa na nyama, sukuma wiki, njegele, karoti na mboga za kila aina. Kutayarisha mapishi haya ni rahisi sana. Haya ni mapishi ya kwanza niliyojifunza nilipokuwa kenya.
Nimeongeza upishi wangu katika mapishi haya; mfano vitunguu vya kukaanga na dhania/majani ya mgiligilani si mapishi ya Githeri, lakini yanapendeza ukila pamoja. Ukitembelea Nairobi, usisahau kula githeri.
Githeri

Ingredients
  • 250g viazi ulaya
  • ¾ kikombe Mahindi mabichi
  • ½ kikombe Njegere mbichi
  • ¼ kikombe vitunguu vya kijani (unaweza kutumia vya kawaida)
  • ½ kikombe karoti zilizokatwa ndogo kama njegere
  • 1 kijiko-mezani Dhania /majani ya mgiligilani
  • Ghee
  • Chumvi
  1. Chemsha, viazi, njegere, mahindi na karoti katika sufuria mbalimbali, usisahau chumvi
  2. Ponda viazi kwenye bakuli kubwa.
  3. Tumia sufuria ndogo kukaanya vitunguu na dhania kwa dakika moja.
  4. Kwenye bakuli hilohilo la viazi, ongeza hivyo vitunguu ulivyopika, na viungo vyote vilivyobaki na kijiko kimoja cha mezani cha ghee.
  5. Weka mezani chakula kikiwa bado chamoto, ongezea vitunguu vya kukaanga.

Kula na :
•Nyama au samaki yeyote unaotaka. Najua sisi waswahili tunapenda michuzi, usitumie mchuzi mwingi au viazi vinaweza vikawa kama uji